Wanawake wa Mradi wa Mzinga wa Nyuki

Kenya

Entashata

Wanawake wa mradi wa mizinga ya nyuki wakisimama karibu na mizinga hiyo. Mradi ulianza wakati Wanawake walipoamua kuwa wanataka kujiwezesha. Walienda Entashata CBO kwa usaidizi na kuanza mradi wa mizinga ya nyuki. Wana akaunti ya benki ambapo huhifadhi mapato yote kutoka kwa asali ambayo wanauza.

“Kupitia mradi huu tumewezeshwa na kujitegemea. Kutokana na kipato tulichopata tumeweza kuwasaidia wasiojiweza na kufadhili watoto wawili kupitia shule.”

Moja ya kero kubwa zinazowakabili ni ukosefu wa vifaa vya kuvunia na wakati mwingine asali huharibika kwa kuwa hawana zana na vifaa vya kuvunia. Wanahitaji viti bora zaidi kwa mizinga yao ya nyuki kwa sababu mchwa hushambulia sehemu walizonazo kwa sasa.

© Esther Sweeney / Ipa

Wanawake wanne wa Mradi wa Mzinga wa Nyuki
Mizinga ya nyuki
Wanawake wa Mradi wa Mzinga wa Nyuki