Christine Lekamario

Kenya

PACIDA

Christine Lekamario na Margaret Leparkry wa Namaiyana Youth Group katika mkutano wa kila wiki wa kikundi cha vijana.

Christine Lekamario wa Namaiyana Youth Group. “Kabla ya PACIDA sikujua kuhusu usafi hasa juu ya umuhimu wa kuchimba vyoo ili kupunguza rsik ya magonjwa. Pia nimejifunza kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na umuhimu wa kupanda miti. Nimejifunza umuhimu wa kutoharibu maji na sasa maji ninayotumia nyumbani ninayasafisha na kuyatumia kwa bustani yangu ya jikoni badala ya kuyamwaga na kuyapoteza.”

Margaret Leparkry wa kikundi cha vijana cha Namaiyana. “Kupitia PACIDA nimefundishwa kuhusu uzazi wa mpango, bustani za jikoni na mabadiliko ya tabia nchi. Pia nimeelimishwa juu ya faida za kumpeleka mtoto wangu kliniki. Hapo awali hatukuwa na uwezo wa kununua pedi za usafi lakini kupitia PACIDA tunapata zinazoweza kufua na tunafundishwa kuhusu usafi na utupaji wa pedi.”

© Esther Sweeney / Ipas

Christine Lekamario
Margaret Leparkry
Christine Lekamario na Margaret Leparkry wa Namaiyana Youth Group katika mkutano wa kila wiki wa kikundi cha vijana.